MAFUNZO KWA AJILI YA WAHUDUMU WA MABASI NA VYOMBO VINGINE VYA USAFIRI

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) kimeandaa mafunzo kwa ajili ya kujenga uwezo wa utendaji kazi wenye tija na ufanisi kwa watoa huduma za usafirishaji.

Walengwa wa Mafunzo

  • Wamiliki wa makampuni ya usafiri na usafirishaji
  • Madereva
  • Makondakta
  • Watoa huduma za usafirishaji wa mizigo
  • Watoa huduma zingine za usafiri zikiwemo Daladala, bajaji, pikipiki nk.

Mada Zitakazofundishwa

  • Sheria na kanuni za usalama barabarani
  • Weledi na maadili kazini
  • Usalama, uokoaji na huduma ya kwanza
  • Huduma kwa wateja
  • Technolojia na huduma za usafiri na usafirishaji
  • Elimu ya biashara, fedha na uwekezaji wenye tija

Muda wa Mafunzo na Ada

Mafunzo yataendeshwa kwa Siku 7 za kazi kwa gharama ya shilingi 200,000/=ambayo italipwa kwa control namba ya malipo ya Serikali.

Namna ya Kujisajili

Bofya link ili kujisajili kuhudhuria mafunzo:

https://docs.google.com/forms/d/1Bu1v7NHAOYaoBJrknjyzjfaReoecRMJyz0nSrAhsAKU/edit

 

Kwa mawasiliano

Piga simu namba 0712793834

Barua pepe: robi.mwema@cbe.ac.tz