Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika kampasi ya Dar es Salaam kwa masomo yatakayoanza mwezi Novemba, 2025 kwa Dirisha la Tatu kuanzia tarehe 06 – 10 Oktoba, 2025 katika program zifuatazo:
Pia Chuo kinaendelea kupokea maombi ya kujiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) katika fani zifuatazo:
Sifa za kujiunga na programu napatikana kwenye tovuti ya chuo pamoja na vitabu vya mwongozo wa udahili (Admission guidebooks).
Dirisha la tatu la maombi kwa ajili ya Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree) litafunguliwa tarehe 06 na kufungwa 10 Oktoba, 2025.
Waombaji watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Chuo www.cbe.ac.tz au fika katika kampasi zetu. Gharama za maombi ya kujiunga ni bure.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
Barua pepe: admissions@cbe.ac.tz
Simu: 0777 151 323
Tovuti: www.cbe.ac.tz
“KARIBU CBE, MABINGWA WA ELIMU YA BIASHARA”