MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA MABASI YA ABIRIA

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE)

MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA MABASI YA ABIRIA

 

Malengo ya mafunzo

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kupitia Sheria ya Udhibiti wa Usafiri ya Mwaka 2019 na Mwaka 2020 zinamtaka kila mhudumu wa vyombo vya usafiri wa umma kupatiwa mafunzo ya msingi kuhusu huduma kwa wateja, huduma ya kwanza, na usimamizi wa operesheni za usafiri. Kupitia mpango huu, Chuo cha Elimu ya Biashara kimepewa jukumu la kuandaa na kutoa mafunzo kwa wahudumu wote wa mabasi ya abiria nchi nzima.

Moduli zinazofundishwa

  1. Sheria, kanuni na maadili
  2. Usalama na uokoaji
  3. Usimamizi wa dharura na huduma ya kwanza
  4. Afya na mazingira
  5. Weledi na huduma bora kwa wateja
  6. Matumizi ya mfumo wa tiketi mtandao

 

Tarehe za mafunzo: 22 – 29 Aprili, 2024

Mikoa husika

  • Dar es Salaam
  • Dodoma
  • Morogoro

Gharama za mafunzo: TZS 200,000.00

Mawasiliano zaidi: Ms. Neema Kitonka (barua pepe: neema.kitonka@cbe.ac.tz; simu: 0782 033350)