UVAAJI WA BARAKOA NA UPIMAJI WA JOTO LA MWILI

Rate this item
(2 votes)
UVAAJI WA BARAKOA NA UPIMAJI WA JOTO LA MWILI

Chu cha Elimu ya Biashara (CBE) kinapenda kuwataarifu wananchi kwa ujumla kwamba kufuatia maagizo ya Serikali kutaka kila mtu achukue hatua za kujikinga na kuzuia maambukizi mapya na kuenea kwa ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwa kuwalinda wahusika pamoja na wadau, CBE inatoa maelekezo yafuatayo:-
1. Kuanzia tarehe 22/04/2020 na kuendelea wanajumuiya/wageni wote watakaolazimika kufika katika ofisi za (CBE) kote nchini kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali watatakiwa kuvaa Barakoa (Mask) kwa lengo la kujikinga wao na wengine.
2. Wanajumuiya/wageni wote wanatakiwa kupima joto, kunawa mikono na kupata vitakasa mikono (Sanitizers) wakati wa kuingia na kutoka kwenye ofisi zetu.
3. Chuo kitaendelea kutoa taarifa na maelekezo kwa wanajumuiya/wageni wote kuhusu hatua za kujikinga na ugonjwa huu kadri itakapobidi.
4. Chuo kitaendelea kuzingatia taadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Corona pasipo kuathiri utendaji wa kazi na kutoa huduma kwa wateja

History of CBE

The COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (CBE) was established in 1965 by the Act of the Parliament. COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION Act No. 31 of 1965. His Excellency, J.K. Nyerere, the first President of the United Republic of Tanzania officially opened the new College in January 1965. The College was officially named the “College of Business Education” (CBE). The said Act of Parliament gives the College its legal status as an autonomous institution with its Governing Body. The College shall be governed and administered in accordance with the provisions of this Act.

CONTACT US

The origin of the College of Business Education (CBE) is closely linked to the history of the Nation itself.

Address : Bibi Titi Mohamed Rd. P. O. Box 1968, Dar es Salaam

Hotline : +255-022-2150177

light arrowCALL FOR PAPERS FOR BEDC2020, SEE DETAILS HERE