METROLOGY DAY

Rate this item
(0 votes)
METROLOGY DAY

 

Chuo kimekuwa kikitoa mafunzo ya Muda mrefu na mfupi kwa wanaoajili na wataalam katika idara za serikali zinazohusika na vipimo na viwango kama vile Wakala wa Vipimo Tanzania, Shirika la Viwango Tanzania, Wakala wa Barabara Tanzania pamoja watalaam wanaohusika na vipimo na uhakiki wa ubora katika viwanda mbalimbali.
Mafunzo haya yana lengo la kufanikisha yafuatayo:
 Kuelimisha kuhusu mifumo ya Vipimo na Viwango.
 Kuonesha mapungufu ya kisera yanavyoweza kusababisha kukosekana kwa taasisi imara, upungufu wa rasilimali watu na fedha hatimaye kusababisha athari za kiafya na uchumi.
 Kushawishi watunga sera na wafanya maamuzi kuboresha sekta ya Vipimo na Viwango ili kusaidia kutekeleza mkakati wa Tanzania ya viwanda.

1.2. Umuhumu Elimu ya Vipimo na Viwango ni nini?
• Kuwezesha usawa katika biashara kwa kutumia kanuni za viwango na ubora zilizo linganifu kikanda na kimataifa na kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa bidhaa za Tanzania.
• Kusaidia kusambaza teknologia ya uzalishaji na upimaji viwandani kwa kuiga teknologia zilizobuniwa na chi zilizoendelea.
• Vipimo na Viwango ni muhimu katika kumlinda mtumiaji wa bidhaa, mbinu za kisasa za vipimo zinaweza saidia upimaji sahihi wa gesi asilia, mita za umeme, pampu za mafuta na vidhibiti mwendo wa magari barabarani.
• Maendeleo ya teknolojia ya vipimo husaidia kupunguza vifo vya wagongjwa wa kansa ambavyo hutokana na matibabu au uchunguzi wa wagonjwa kwa kutumia mionzi mikali ya X-ray.
• Kuelewa vizio vya vipimo. Kwa mfano bidhaa iliyofungashwa yenye uzito wa kilogram 1 katika nchi fulani itadumu kuwa hivyo ikipimwa katika nchi yoyote.

1.3 Umuhimu wa serikali kusaidia/ Kufadhili elimu ya Vipimo na Viwango
Huduma bora kwa jamii ni kitu ambacho kila mtu anategemea kutoka serikalini na lazima zipatikane kwa ustawi wa taifa. Katika hali ya kawaida, jamii inategemea huduma kama maeneo ya michezo, taa za barabarani, jeshi la ulinzi na usalama n.k.

Katika muktadha wa ubora wa bidhaa za viwandani, jamii inategemea yafuatayo:
 Taasisi zilizoimarika kwa vitendea kazi na wataalamu wenye weledi katika kulinda jamii dhidi ya bidhaa hafifu.
 Uwepo wa taasisi inayotoa mafunzo kwa wataalamu na kufanya tafiti katika nyanja za vipimo na teknolojia zake katika sekta za biashara,afya na ulinzi wa mazingira.
 Kuwa na sera ya vipimo/miundombimu ya vipimo na viwango inayojumuisha mamlaka mbalimbali zinazohusika kumlinda mlaji.
 Uwepo wa sheria na kanuni linganifu na nchi nyingine zinazotumika katika kuandaa nyaraka za ubora, uhakiki wa vipimo, uthibiti wa vipimo, ukaguzi wa vipimo pamoja na bidhaa.

1.3. Gharama na faida za kuwa na taasisi zenye uwezo wa kuhakiki vipimo ndani ya nchi.
Kampuni ya Daiwoo Shipbuilding & Marine Engineering ya Korea ilitumia dola za Marekani zipatazo 41,000 (Tsh 98,400,000) kwa kupeleka vipimo vyao nchini Marekani ili vikahakikiwe, lakini kifaa hicho hicho kilipohakikiwa(calibration) na maabara ya Korea kiligharimu kiasi cha dola za Marekani 30,000 (Tsh72,000,000) hivyo basi, kampuni iliweza kuokoa kiasi cha Tsh 26,400,000

2.0 UJUMBE MAALUM KWA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA SIKU VIPIMO DUNIANI

Uwezo wa uzalisaji wa bidhaa za viwandani na huduma za kibiashara hutegemea fursa zilizopo na uwezo wa kiushindani katika soko la dunia na ushishiki katika ongezeko la mnyororo wa thamani wa bidhaa. Lakini changamoto kubwa kuifikia fursa hizi huwa ni ugumu wa kuonesha uwezo wa kukidhi ubora na viwango vilivyowekwa kimataifa. Ili kujikwamumua na changamaoto hii ya vikwazo vya ubora wa bidhaa hakuna budi Tanzania kama taifa lenye nia ya kuitumia fursa ya soko la dunia ijikite kuifamu elimu ya vipimo na viwango ambayo ndiyo injini ya uhakiki wa ubora wa bidhaa zinazodhitiwa na mamlaka mbalimbali za serikali. Mamlaka hizi lazima ziunganishwe na dira moja wakati wa uundaji wa sera ya Miundombinu ya Ubora (Quality infrastructure).

Vilevile Miundombinu ya Ubora hutegemea elimu ya vipimo na viwango ambayo inawezesha kufanikisha utendaji katika shughuli za mambo ya ithibati, uhakiki wa bidhaa na usimamizi wa ushindani sawa katika soko huru.
Mamlaka mbalimbali za udhibiti zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na Viwango vya mashirika ya kimataifa na kikanda na nchi kutegemea sekta husika. Kanuni hizi ni mwongozo wa kiufundi na teknolojia, busara na uzoefu uliopatikana katika kada mbalimbali.
Mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa kuunda taasisi za vipimo na viwango ni yafuatayo:
• Sera
• Sheria
• Kanuni
• Utawala
• Kuhusisha sekta (sekta ya umma na binafsi)
• Rasilimali fedha (Sera lazima itaje chanzo cha mapato cha taasisi kama ni tozo kutokana na huduma wanazotoa au ruzuku kutoka serikalini.)

 
2.1 NGUZO KUU NNE MUHIMU ZINAZOWEZESHA KUUNDA SERA YA MIUNDOMBINU YA UBORA NA KUIWEZESHA NCHI KUSHIRIKI KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA
Ifahamike kwamba ili nchi ipate maendeleo ya kiuchumi lazima ifanye biashara na mataifa mengine. Na ili nchi iweze kufanya biashara na mataifa mengine lazima ikidhi vigezo vya kiufundi katika bidhaa zinazozalishwa viwandani.
Nguzo hizo tofauti zikishirikiana ziinaunda Miundombinu ya ubora na kuleta maendeleo endelevu kwa kuwa zitasaidia kukidhi vigezo vya biashara ya kimataifa.
Nguzo hizi ni kama zifuatazo:
• Viwango (Standardization);
• Vipimo (Metrology);
• Uhakiki wa ubora (Conformity Assessment);
• Ithibati (Accreditation).

 

2.1.1 Vipimo (metrology)
Huimarisha upimaji sahihi, unaoaminika na linganifu kimataifa katika sekta zote.Vipimo vimegawanyika katika mkundi yafuatayo:
 Vipimo vya kisayansi
 Vipimo vya viwandani
 Vipimo vitumikavyo kibiashara, afya, usalama na mazingira. (Legal metrology)

Vipimo vya kisayansi (Scientific metrology)
Vipimo vya kisayansi hufayanywa na taasisi huru ( Metrology institute).Kazi kubwa ya taasisi hii ni kufanya utafiti wa vipimo na mbinu bora za upimaji kwa usahihi wa hali ya juu, kutunza vipimo linganishi (calibration standards) kuwa na maabara bora.Taasisi hizi mara nyingi huwa katika nchi zilizoendelea kiuchumi. Kwa mfano nchi ya Ujerumani kuna taasisi inayoitwa Physikalisch-Technische Bundesanstalt (PTB)

Vipimo vya Viwandani (Industrial metrology)
Mara nyingi aina hii ya vipimo hutekelezwa na Shirika la Viwango ambalo jukumu lake ni kuchapisha nyaraka za viwango na kufanaya huduma ya kulinganisha vifaa vitumikavyo kupima viwandani wakati wa uzalishaji. Kimsingi viwango vinavyoandaliwa na shirika hili ni vya hiari (voluntary standards). Isipokuwa viwango hivi vitakuwa lazima kutekelezwa endepo tu vimeingizwa katika kanuni. (Technical regulations). Kwa hiyo wazalishaji viwandani na watoa huduma wanatakiwa kuuziwa nyaraka za viwango na kupewa huduma ya kufanyiwa ulinganifu (calibration) wa vifaa vyao vitumikavo kupima, pia kufanyiwa uhakiki kama bidhaa zilizozalishwa kiwandani zimekidhi viwango husika (product certification). Kwa nchi yetu jukumu hili hufanywa na Shirika na viwango la Taifa (TBS).

Vipimo vitumikavyo kisheria (Legal metrology)
Aina hii ya vipimo hudhibitiwa/husimamiwa na taasisi ya serikali ambayo ni nyenzo kuu ya kudhibiti vipimo na vifaa vya kupimia katika nyanja za biashara,utii wa sheria ya vipimo,uhakiki wa vifaa vya tiba na ulinzi wa mazingira. Pia taasisi hii inapewa nguvu ya kisheria kukamata na kuzuia vipimo vyote visivyokidhi viwango. Kwa nchi yetu taasisi hii huitwa Wakala wa Vipimo. Taasisi hii tufanya majukumu ya kusimamia sheria, kanuni na viwango ambayo siyo vya hiari (compulsory standards or technical regulation)
Huduma zitolewazo na taasisi hizi ni pamoja na zifuatazo.
• uthibiti wa mawe ya mizani
• uthibiti wa mizani
• uthibiti wa mita mafuta bandarini na vituo vya mafuta
• ukaguzi wa mita za umeme
• uthibiti wa mita za maji
• uthibiti wa vifaa tiba
• ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa
Taasisi hii inahitaji watumishi wake wawe wenye weledi mkubwa kwenye fani ya vipimo na pia wawe wamebobea kwenye fani ya sheria ya vipimo.Watumishi wa taasisi hii katika utendaji wao wa kila siku hutumia sheria iliyotungwa na bunge na kanuni mbalimbali ambazo ni za kiufundi na teknolojia ya juu katika ugaguzi wa vipimo na bidhaa zilizofungashwa.
Bila kuwepo kwa vipimo na vifaa vya kupimia vizio uzito, urefu, ujazo na joto hakuna biashara inayoweza fanyika kwa usawa bila ya upunjaji.
Vipimo vina husisha sheria na kanuni husika katika kumlinda mlaji wa bidhaa. Shughuli mahususi katika vipimo ni pamoja na ukaguzi wa mizani za biashara, mizani za barabarani, pumpu za mafuta gesi na matanki ya kuhifadhi mafuta nchi kavu , matanki ya mafuta kweye meli na mita zake, mita za mafuta bandarini,mita za maji na umeme.

Sheria za vipimo zinawapa nguvu watendaji waliopo ndani ya mamlaka husika kukusanya maduhuli ya serikali au kukusanya tozo endapo mtumiaji wa vipimo au mmilikiwa kifaa cha kupia amekiuka sheria. Si hivyo tu bali sheria hizo zinawapa nguvu watendaji hao kushikilia na kutaifisha vipimio ambavyo ni batili na kuzuia bidhaa zilizofungashwa zikiwa hafifu.
Viwango vya vipimo ninavyo andaliwa na mamlaka za vipimo husaidia kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika sekta za uchumi, afya, amazingira na usalama.

2.2.2 Viwango (standardization)
Viwango ni nyaraka zinazoandaliwa na shirika la viwango la taifa. Nyaraka hizi husambazwa kwa kuwauzia wamiliki wa viwanda au watoa huduma ili waweze kuzalisha bidhaa na huduma zinazokidhi vigezo vya nchi au kimataifa. Shirika la viwango la taifa (TBS) ndilo linalohusika kuandaa nyaraka za viwango na kusambaza na kuwauzia wadau husika.

2.2.3 Uhakiki wa ubora wa bidhaa (conformity assessment).
Uhakiki wa bidhaa hufanywa na mamlaka za serikali au kampuni binafsi ambazo zimepata ithibati ya kimataifa kufanya kazi hiyo. (Mfano wa kampuni binafsi ni Intertek na SGS)
Kazi hii hufanywa kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na viwango vinavyo simamiwa taasisi za vipimo na viwango.Taasisi za vipimo na viwango zinaweza kufanya kazi hii ya uhakiki wa ubora zenyewe au zikagatua madaraka kwa kampuni binafsi zilizokidhi vigezo.
Jukumu la uhakiki wa ubora wa bidhaa hufanywa na makundi yafutavyo:
• Mzalishaji au msambazaji wa bidhaa au huduma.
• Mnunuzi au mpokeaji wa bidhaa au huduma
• Kundi la tatu ambalo halihusiki katika biashara.(third party)
Jukumu la kundi hili ni kuhakikisha kuwa hakuna bidhaa hafifu inayoingia sokoni. Katika mchakato huu hufanyia ukaguzi na majaribio ya bidhaa husika kwa kufuata viwango vilivyowekwa. Endapo itathibika bidhaa imekidhi viwango afisa mkaguzi atataoa hati ya kudhi viwango. Mara nyingi kundi hili hufanya kazi sana katika nchi zinazoendelea.

2.2.4. Ithibati (Accreditation)
Ithibati ni mchakato wa kutathmini uwezo taasisi au mtu anayetoa huduma ya uhakiki (conformity assessment), hati ya ubora wa bidhaa (product certification) ulinganifu wa vifaa vya kupimia (calibration).
Lengo kuu la nguzo hii ya ubora ni kuwa na uhakika kuwa mtoa hudumu anao umahiri wa kufanya kazi hiyo.


3.0 Taasisi mahususi za utoaji wa mafunzo ya vipimo na viwango
Jukumu la taasisi hii ni kutoa mafunzo, kutoa huduma kwa jamii na kufanya tafiti za kisayansi kuhusu teknolojia mpya za upimaji. Nguzo zote zilizotajwa hapo juu haziwezi kutekeleleza majukumu yake kwa ufanisi endepo maafisa watendaji hawana ujuzi wa kutosha. Aina za mafunzo inaweza kuwa ya muda mfupi au muda mrefu.
Chuo cha elimu ya Biashara (Cbe) ni chuo pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki, na kati ambacho hutoa mafunzo ya elimu ya vipimo katika ngazi za cheti, astashahada, shahada na shahada ya juu.

4.0 ATHARI ZA KUKOSEKANA KWA SERA YA TAIFA YA MIUNDOMINU YA UBORA
Katika nchi yetu kuna taasisi mbalimbali ambazo zinahusika kusimamia kanuni za ubora za kisekta au kiidara au kiwizara. Lakini kila taasisi imejipanga kila moja pekeyake na hatimaye kupelekea kukinzana au kuingiliana badala ya kushirikiana. Matokeo hasi ya utendaji wa taasisi hizi yamepelekea Tanzania kwa kiasi kikubwa kushindwa kuzalisha bidhaa zinazokidhi ubora wa kikanda na kimataifa.
Suluhisho la tatizo hili ni kuunda sera ya Taifa Miundombinu ya Ubora wa bidhaa ambayo ndiyo dira ya taasisi zote zinazoshiriki katika kuunda na kusimamia kanuni za ubora ili kufikia viwango vya kimataifa na kuviwezesha viwanda vya ndani kukidhi matakwa ya soko la dunia.

5.0 JUKUMU LA SERIKALI KATIKA KUUNDA NA KUTEKELEZA SERA
Serikali inatakiwa kujipanga upya katika kuunda na kutekeleza sera hii ya Taifa badala ya kuiachia taasisi moja ambayo itapenda kujinufaisha kwa kipato na kuzishinda taasisi nyingine ambazo zilikuwa zikigongana kimaslahi.
Serikali inawajibika kuunda sera ya ubora na kuhakikisha kuwa mamlaka za udhibiti za kisekta zitatekeleza malengo ya sera hii kwa kukidhi matakwa ya nchi kwa kuendena na mwenendo wa biashara ya kimataifa.
Kwa kifupi mamlaka mbalimbali za udhibiti zinazounda miundimbinu ya ubora zinatakiwa ziundiwe kanuni ya pamoja.
Tunapendekeza kuwa Wizara mojawapo tu ndiyo iwe msimamizi mkuu wa sera hii. Kwa kuzingatia uzoefu wa nchi nyingine, Wizara ya Viwanda ya Biashara na Uwekezaji ndio iwe msimamizi mkuu wa sera hii kwa kuwa wizara hii ina uzoefu na imekuwa ikihusika kusaini mikataba ya shirika la biashara la kimataifa (WTO). Pendekezo la pili ni kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuweza kuisimamia kwa kuwa maagizo yaWaziri mkuu yatatekelezwa na watumishi na mawaziri mbalimbali ambao taasisi zilizopo chini ya wizara zao zitahusishwa katika sera hii.

Kimantiki, jukumu la mamlaka ya udhibiti ni kuhakiki waingizaji wa bidhaa sokoni wanaonesha ushahidi wa kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini au kuzalishwa zimekidhi viwango vya ubora kwa kuonesha nyaraka za ukaguzi. Sera itamke wazi kuwa mwagizaji wa bidhaa uwe huru kuchagua tasisi yoyote ya ukaguzi yenye vigezo kufanya kazi hiyo ya uhakiki (testing and certification) badala ya kazi hiyo kufanywa na mamlaka ya uthibiti. Hii itasadia mfanyabiashara kutopoteza muda mwingi kuisubiri mamlaka moja peke yake ifanye kazi hiyo, pia itapunguza gharama ya uhakiki wa bidhaa kwani kutakuwa na ushindani wa biashara na kupelekea punguzo la bei.


6.0 MIFANO YA NCHI ZILIZO CHUKUA HATUA KUANZISHA SERA MADHUBUTI YA UBORA NA VIPIMO
Tukinukuu kutoka kwenye ripoti ya shirika la maendeleo la viwanda duniani, (UNIDO) Jambo kuu ni kuwa na sera Miundombinu ya ubora ambayo inajumuisha maabara za uhakiki zinaendeshwa na taasisi mbalimbali kama ilivyoinishwa hapa chini.
 Taasisi ya vipimo ya taifa (national metrology institute)
 Taasisi ya huduma ya ulinganishi wa vipimo (national calibration service)
 Maabara mbalimbali za ulinganishi zinazoendeshwa na sekta ya umma na sekta binafsi.
 Ofisi ya wa Wakala wa Vipimo.
Jambo la msingi hapa ni kwamba maabara zote zinafanaya uhakiki na majaribio lazima ziwe na sifa ya ithibati kwa kiwango cha ISO/IEC 17025.
Mfano wa nchi zinazoendelea zilizochukua hatua ya kuaanzisha sera ya miundombinu ya ubora.
 Sri Lanka
 Nepal
 Vietnam
 Mongolia
 Guyana
 Botswana

Faida zilizopatikana kutokana na sera hii.
 Taasisi nyingi zimeweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku ya serikali.
 Wajasiliamali wengi wadogo na wakubwa waliweza kulifikia soko la nje kwa kuwa maabara zenye ithibati zilifanya uhakiki wa bidhaa zao.
 Ukaguzi wa bidhaa ulifanyika kwa muda mfupi zaidi
 Gharama za ukaguzi wa bidhaa za ndani zilifanyika kwa gharama ndogo Zaidi
 Uzoefu wa ukaguzi na uhakiki wa bidhaa ulisambaa kwa watu wengi.
7.0 HITIMISHO
Chuo cha Elimu ya Biashara ni hazina kubwa ya taifa kwa kuwa kina uzoefu katika sekta ya biashara Zaidi ya miaka 54.Kwa kutumia uzoefu uliopatikana kwa miaka yote hii, tunaweza kushiriki kaijenga Tanzania ya Viwanda kwa kufia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kuzalisha wataalamu wa Vipimo na Viwango pamoja na kufanya tafiti katika sekta za biashara na viwanda.

History of CBE

The COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (CBE) was established in 1965 by the Act of the Parliament. COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION Act No. 31 of 1965. His Excellency, J.K. Nyerere, the first President of the United Republic of Tanzania officially opened the new College in January 1965. The College was officially named the “College of Business Education” (CBE). The said Act of Parliament gives the College its legal status as an autonomous institution with its Governing Body. The College shall be governed and administered in accordance with the provisions of this Act.

CONTACT US

The origin of the College of Business Education (CBE) is closely linked to the history of the Nation itself.

Address : Bibi Titi Mohamed Rd. P. O. Box 1968, Dar es Salaam

Hotline : +255-022-2150177

light arrowCALL FOR PAPERS FOR BEDC2020, SEE DETAILS HERE