New events
MARCH INTAKE 2022-2023
You are all welcome to APPLY for various courses in march intake for the year 2022/2023.
CBE ZANZIBAR
CBE KUTUA ZANZIBAR KWA KISHINDO
Wajumbe wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) pamoja na viongozi wa chuo leo 17/ 03/ 2022 wametembelea eneo la Chuo lililopo Chwaka - Zanzibar ambapo ujenzi wa Kampasi ya tano utafanyika hivi karibuni.
Wajumbe wa Bodi na Uongozi wa Chuo pia walipata fursa ya kukutana na Mbunge wa Chwaka Mhe. Haji Mlenge ambaye alieleza matarajio ya wananchi wake juu ya ujio wa Chuo hicho kikubwa cha Biashara nchini.
Aliwaomba viongozi wa Chuo kuharakisha mchakato huo ili wananchi wake waweze kunufaika kijamii na kiuchumi kwani shughuli za kiuchumi zitaongezeka na kuwaongezea wananchi kipato.
Alieleza kuwa faida nyingine ni kuwapunguzia wazazi na walezi gharama ambao hulazimika kuwasomesha vijana wao Tanzania bara.